Ijumaa 9 Oktoba 2026 - 13:35
Dalili za Athari Kubwa za Kamandi ya Polisi Zimejitokeza Wazi Zaidi Katika Vita vya Hivi Karibuni/ Usalama nchini unatokana na ushujaa na ujasiri wa vikosi vya Polisi

Hawza/ Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Polisi, amesema: “Usalama ni miongoni mwa neema muhimu zaidi za Mwenyezi Mungu. Kuwepo usalama katika maeneo mbalimbali ya Iran yetu tukufu, kuanzia miji mikubwa hadi vitengo vidogo kabisa vya makazi ya watu katika vijiji na mitaa; kuanzia ulinzi mgumu wa mipaka katika mazingira magumu ya hali ya hewa na maeneo mbalimbali ya kijiografia, kuanzia milimani hadi baharini, kutoka nyanda za wazi na misituni hadi maeneo ya katikati kabisa ya nchi, kunatokana na ushujaa na ujasiri wa vikosi vya kujitolea na vinavyofanya kazi kwa bidii vya Polisi, ambavyo ni mojawapo ya nguzo imara za usalama wa nchi.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Vikosi Vyote vya Majeshi, kwa mnasaba wa Wiki ya Polisi, ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Usalama ni miongoni mwa neema muhimu zaidi za Mwenyezi Mungu. Kuwepo usalama katika maeneo mbalimbali ya Iran yetu tukufu, kuanzia miji mikubwa hadi vitengo vidogo kabisa vya makazi ya watu katika vijiji na mitaa; kuanzia ulinzi mgumu wa mipaka katika mazingira magumu ya hali ya hewa na maeneo mbalimbali ya kijiografia, kuanzia milimani hadi baharini; kutoka nyanda za wazi na misituni hadi maeneo ya katikati kabisa ya nchi, kunatokana na ushujaa na ujasiri wa vikosi vya kujitolea na vinavyofanya kazi kwa bidii vya Polisi, ambavyo ni mojawapo ya nguzo imara za usalama wa nchi.

Usalama huu huwezesha kuwepo nyanja mbalimbali za kijamii na kimaadili, pamoja na hali ya utulivu na ustawi wa umma ndani ya jamii. Huduma hii yenye thamani kubwa, mbali na kuwa ni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, pia inaungwa mkono na jamii kwa kiwango kikubwa.

Jukumu muhimu la Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika ngazi mbalimbali, kuanzia safu za uongozi na makao makuu hadi vituo vya polisi na vituo vidogo vya ulinzi, katika kuhakikisha usalama, limezidi kujitokeza wazi katika miaka ya hivi karibuni. Dalili za athari za jukumu hili zilijitokeza wazi zaidi katika vita vya kulazimishwa vya pili na vya tatu.

Kujikita adui mhalifu wa Marekani na Mzayuni, pamoja na msisitizo wake wa kushambulia safu mbalimbali za Kamandi ya Polisi, kuanzia ngazi za juu kabisa hadi vikosi vyake vya chini kabisa, pia kumeweka wazi zaidi umuhimu wa taasisi hii.

Hata hivyo, juhudi hizi za kukata tamaa na mashambulizi haya maovu yaliyolenga nguzo za utulivu na usalama wa jamii, ambayo hayana mfano wake katika historia, hazikuwafanya askari jasiri wa Kamandi ya Polisi kupunguza hata kidogo utekelezaji wa majukumu yao. Bali, hata wakiwa mitaani na ndani ya magari, waliendelea kutekeleza majukumu na wajibu uleule waliokuwa wakiutekeleza katika maeneo yao ya kazi na kwenye vituo vyao.

Kwa sababu hiyo, taifa la Iran, ambalo limekandamizwa lakini lina nguvu, linatambua na kuthamini juhudi na kazi zisizokoma za watumishi wanaolinda usalama wa nchi. Kwa upande mwingine, vikosi vya Polisi, ambavyo kama Jeshi na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), vinatokana na jamii yenyewe, vinaweza kuongeza imani ya wananchi kwa taasisi hii yenye thamani kupitia mwenendo wao unaojenga uaminifu.

Mara nyingi, juhudi na kujitolea walinzi wa usalama huenda vikachukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni mambo ya kawaida. Hali hii ya kudhulumiwa na kutotambulika ndiyo inayozidisha malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kuimarishwa vikosi vya kulinda usalama katika nyanja zote, ikiwemo rasilimali watu, vifaa na mifumo ya kiteknolojia, hususan kuboreshwa teknolojia, pamoja na matumizi yenye malengo maalumu ya akili mnemba katika uchanganuzi wa data, kuna nafasi muhimu katika kuboresha ubora na kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu awapandishe daraja na awajaalie radhi zake za milele mashahidi wenye vyeo vya juu wa Kamandi ya Polisi. Pia, ninatoa shukrani kwa familia zote, wafanyakazi, wanajeshi wa kujitolea na vikosi jasiri na vyenye moyo wa kizalendo, hususan kamanda jasiri, asiyechoka na mwenye akili nyingi wa Kamandi ya Polisi, pamoja na juhudi zake kubwa za kujitolea.

Ninatumaini kwamba, kwa dua za Bwana wetu, Imam Mahdi (ajjalallahu ta‘ala farajahu sharif), wataendelea kufanikiwa zaidi katika kuinua hadhi ya usalama, nguvu na heshima ya Iran.

Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha